Dkt. Kumbuka atangaza kuwa shabiki wa Simba akitokea Yanga




Msanii na Mtangazaji wa kituo cha radio cha EFM, Dkt. Kumbuka ametangaza rasmi kuwa shabiki mpya wa klabu ya Simba SC akitokea Yanga.

Kumbuka ametangaza uwamuzi huo leo April 20, 2021 wakati klabu hiyo ikisaini mkataba wa miaka mwili wa Shilingi bilioni mbili na kampuni ya Vunja Bei Group kwa ajili ya kutengeneza na kusambaza jezi za Simba SC.

“Ukiwa Simba unapata raha sana. Nimeamua kuwa chawa gegedu wa Vunja Bei na chawa gegedu wa Simba SC” alisema Kumbuka.

Dkt. Kumbuka anakuwa msanii wa pili kuahamia Simba akitokea Yanga baada ya msanii wa singeli Dulla Makbila kufanya hivyo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad