Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango atoa agizo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba kuanza kushughulikia utatuzi wa masuala ya kifedha katika pande mbili za muungano.
Akizungumza mara baada ya uapisho wa Mawaziri na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Mpango amesema agizo hilo alipewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu na kwa vile mrithi wa Wizara ya Fedha ameshapatikana ataanza na kazi hiyo pamoja na Waziri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo.
"Jana nilikaa nikitafakari agizo lako hasa huyu mchawi ambaye amekuwa anashindwa kutatau masuala ya mahusiano ya kifedha katika pande zote mbili za muungano sasa nimepewa huyo mtoto nimepewa huyo mtoto nifanye hiyo kazi, sasa nimepata mrithi Mhe. Rais nakushukuru sasa nimepata mrithi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba hii ndo iwe kazi kazi yako ya kwanza," alisema Dkt. Philip Mpango.
Aidha, Dkt. Mpango ameahidi kufuatilia kwa ukaribu juu ya mvutano uliopo baina ya mawaziri na manaibu waziri, na kuwaagiza mawaziri kuwapatia kazi za kufanya manaibu waziri huku akimuagiza Katibu Mkuu Kiongozi kwenda kushughulikia tatizo kama hilo kwa makatibu wakuu na manaibu katibu wao.
"Mhe. Rais ulikemea kwa nguvu utaratibu wa mawaziri na naibu waziri kuvutana vutana natumaini walisikia na hili tutalifuiatilia, tunajenga nyumba moja hakuna sababu ya kuvutana," alisema Dkt. Philip Mpango.