Facebook yapiga marufuku 'sauti ya Trump' kwenye mtandao wake





Mtandao wa Facebook umeondoa video ya aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump kwenye ukurasa wa mkwe wake.


Facebook ilimpiga marufuku Bwana Trump kutumia mtandao wake mnamo mwezi Januari, kufuatia ghasia zilizosababishwa na wafuasi wake katika jengo la Capitol mjini Washington.



Lara Trump, mchambuzi mpya wa shirika la habari la Fox News, aliweka video ya yeye mwenyewe akimhoji Bwana Trump kuhusiana na masuala mengi tu.



Baadaye, aliweka kwenye mtandao huo, picha ya barua pepe aliyopokea kutoka mtandao wa Facebook ukimuonya kwamba utampiga marufuku kutumia mtandao huo.



Lara Trump, ambaye ameolewa na kijana wa Trump Eric, badala yake aliweka mahojiano hayo katika kipindi chake mwenyewe mtandaoni 'The Right View' katika mtandao wa video wa 'Rumble' na akaiunganisha na ukurasa wake wa Facebook.



Mfuasi wa muda mrefu wa Trump ambaye pia ni mwendeshaji wa kipindi kimoja katika Televisheni ya Fox News Sean Hannity, alielezea hatua hiyo kama "udhibiti wa kupitiliza" kwenye mtandao huo.



Kupigwa marufuku kwa akaunti ya Bwana Trump Januari, 7, siku moja baada ya ghasia zilizotokea bungeni - kunapitiwa tena na bodi ya mtandao huo, ambayo ilianzishwa kujadili maamuzi tata yaliyofanyika.



Akitetea marufuku hiyo wakati huo, Mkuu wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerburg alisema: "Tunaamini hatari ya kumruhusu rais kuendele kutumia huduma zetu kipindi hiki ni ya busara."



Donald Trump pia alipigwa marufuku kutumia mtandao wa Twitter na YouTube.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad