Gwajima Aliamsha: Nape Umenidukua, Tunahitaji Ajenda ya Taifa




Mbunge wa Kawe (CCM), Josephat Gwajima ametaka Tanzania kuweka tafsiri ya maendeleo ambayo kila rais atakayeingia madarakani atatakiwa kuitekeleza jambo alilodai kuwa litasaidia kile alichokiita “kulia” ikiwa nchi itapata kiongozi ambaye hayupo sawasawa.

 

 

Gwajima ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 15, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

 

 

Amesema nchi za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania haziwezi kuendelea kwa kasi kwa sababu hazina mwendelezo wa awamu moja kwenda nyingine kwamba kila rais aliyeingia madarakani anakuwa na namna yake kuhusu maendeleo na kuhoji nchi itaendeleaje kama awamu hizo hazitafanana.

 

 

“Ili tuendelee tunahitaji ajenda ya Taifa. Lazima tu-difine (tutafsiri) maendeleo ya Tanzania kwa miaka 30 ama 50 tuwe na vitu tunaita maendeleo,” amesema.

 

 

Amesema kila rais anayeingia madarakani kwa namna yake na kwa sarakasi yake anakuta vitu vimetafsiriwa kama maendeleo na kuvitimiza kwa namna yake.

 

 

“Kama hatujafanya hivi tuna hatari yake kwa sababu katiba yetu inampa nafasi kila rais anayeingia madarakani kwa namna yake, kwa hekima yake na kwa namna ya kutafsiri yeye maendeleo ya Tanzania,” amesema.

 

 

Huku akisema kuna siku Taifa litapata mtu ambaye si sawa na litalia amesisitiza, “Ikiwa ni nia yetu tuendelee tuwe na vision (malengo) ya miaka 50 ya Taifa, tuitafsiri kama ni kila nyumba iwe na maji ama tupate umeme…, halafu tuseme kila rais anapoingia madarakani katika ilani yake ya chama ijumuishe mambo ambayo tumejiwekea kama maono ya Tanzania.”

 

 

“Kuna mtu atakuja kumuuliza mwenyekiti wa CCM na Amri Jeshi Mkuu kuwa hutakiwi kufanya hivi hayupo huyo? Lakini tutakapokuwa na vision kwamba tunatakiwa kuarchive hiki na kile iwe ni kijani iwe ni nini utatimiza yale ambayo tumejiwekea kama maono ya Taifa letu.”

 

 

Huku akisema kuna siku Taifa litapata mtu ambaye si sawa na litalia amesisitiza, “ikiwa ni nia yetu tuendelee tuwe na vision (malengo) ya miaka 50 ya Taifa, tuitafsiri kama ni kila nyumba iwe na maji ama tupate umeme…, halafu tuseme kila rais anapoingia madarakani katika ilani yake ya chama ijumuishe mambo ambayo tumejiwekea kama maono ya Tanzania.”

 

 

“Kuna mtu atakuja kumuuliza mwenyekiti wa CCM na Amri Jeshi Mkuu kuwa hutakiwi kufanya hivi hayupo huyo? Lakini tutakapokuwa na vision kwamba tunatakiwa kuarchive hiki na kile iwe ni kijani iwe ni nini utatimiza yale ambayo tumejiwekea kama maono ya Taifa letu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad