Moja kati ya principle yangu ya Maisha ni kutoingilia ugomvi kati ya mtu na mtu..Kama ugomvi haunihusu, huwa nakaa neutral kabisaa maana unaweza kujitoa muhanga halafu kesho ukaumbuka.
1. IBRAH
Sijui kama aliwaza mara mbili kabla ya kufanya alichofanya..sijui kama alijaribu kuifikiria nafasi yake katika maisha ya mziki, au ameamua kuitumia hii nafasi ili atrend. Sijui aliwaza nini ila nina uhakika 100% kuwa AMEKOSEA SANA. Ni kijana mdogo sana na ambae bado anapambana kuikuza talent yake kwenye mziki. Bado anahitaji support ya wadau ili afike mbele zaidi kimziki. Sina uhakika hata kama amewahi kufanya show yake mwenyewe bila kuwa na wasanii wengine. Sina uhakika!
Amepata wapi ujasiri wa kununua ugomvi kiasi hiki?, Hata kama yupo upande wa Boss wake, busara yake kubwa ilikuwa ni kukaa kimya. Mbona country Boy kakausha.. Lakini kuanzia sasa 'amenunua' ugomvi na amejiweka kwenye presha kubwa sana ambayo inaweza kumharibia hata kwenye career yake ya mziki. Leo yupo hapo je kesho akitoka/akitolewa, haoni kama anaweza kuwahitaji miongoni mwa hao aliowatukana kwa namna moja ama nyingine? au amesahau kuwa usitukane mamba kabla hujavuka mto?...A very big mistake has been done by Bwana mdogo.
2. BABA LEVO
Yes, unajiita chawa pro max..ni vizuri kwasababu unatetea ugali kwa boss wako. Lakini sijawahi kuona sababu ya baba levo kuingia na kununua ugomvi usiomhusu. Mbona kuna wafanyakazi wenzake wengi tu hapo ofisini na hawajawahi kununua ugomvi wa boss wao? au anazani wao hawana akili?..He is wrong. Unaweza kusimama upande wa Boss wako ila sio kwa namna ambayo baba levo ameiamua. Kila adui wa boss wake nayeye ni adui yake.. kwani kuna ulazima wa kufanya hivyo?..Hivi haoni kama anajiharibia hata heshima yake kwa wengine..Leo anaweza akaona kuwa anafaidika pasipo kujua anakula mtaji wa siku zijazo..Ikitokea ametoka au ameondolewa hapo alipo, haoni kama atakosa pa kuificha sura yake kutokana na kujiharibia kwa watu wengine..Kwanini ujidhalilishe na kujiharibia brand kisa tu unataka umfrahishe boss wako ambae mmekutana ukubwani ..Leo utashangiliwa ila pasipo kujua kuwa unajiharibia..Hao wanaogombana ni kama ndugu maana wanajuana na wanafahamiana siri zao nyingi tu kulingana na ukaribu waliokuwa nao..au baba levo umesahau kuwa ndugu wakigombana inabidi ushike jembe ukalime?
Mifano ipo mingi sana ya kujifunza, Nakumbuka 2012 Dogo janja alitoka kwa madee na akatoa ngoma moja kali sana ya kuidiss management yake ya zamani, lile lilikuwa ni kosa kubwa sana alilolifanya (pengine hadi leo analijutia) maana alikoenda mambo yalikuwa tofauti na matarajio ikabidi arudi 'nyumbani' kwa aibu na bahati nzuri kwake ni kuwa walimsamehe pengine waliamini utoto ndio ulimsumbua..Najua situation ya dogo janja na hizi za baba levo na Ibrah ni tofauti ila zote zinatuonesha kuwa BUSARA NI KUKAA KIMYA maana hatujui labda siku moja tukaihitaji heshima yetu au watu tuliowapoteza kutokana na midomo yetu.