Japan yatangaza hali ya dharura dhidi ya Covid-19





Waziri Mkuu wa Japan Suga Yoshihide alitangaza kuwa hali ya dharura itatekelezwa katika mikoa 4, pamoja na mji mkuu wa Tokyo, katika wigo wa hatua za kupambana na janga la corona (Covid-19).

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Waziri Mkuu Suga alisema kuwa kwa sababu kesi za maambukizi ya Covid-19 zinaendelea kuongezeka, hali ya dharura itatekelezwa katika mji mkuu wa Tokyo pamoja na majimbo ya Osaka, Kyoto na Hyogo.

Akieleza kwamba alichukua uamuzi huo baada ya pendekezo la Kamati ya Ushauri ya serikali ya Covid-19, Suga alitoa wito kwa magavana wa mikoa 4 kuongeza hatua dhidi ya janga hilo.

Akiashiria kipindi cha likizo ya "Oogon Shuukan" (Wiki ya Dhahabu) kati ya Aprili 29 na Mei 5, Suga alisema,

"Lazima tuchukue hatua kali kwa kuzingatia kuenea kwa virusi wakati umma uko kwenye likizo."

Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Covid-19 Shigeru Omi pia alitangaza kuwa hali ya dharura ingeongezwa muda zaidi ikiwa hali ya kupungua kwa kesi haingeweza kuonekana.

Hali ya dharura ambayo itaanza kutekelezwa Jumapili usiku, Aprili 25, katika mji mkuu wa Tokyo pamoja na Osaka, Hyogo na Kyoto, itaendelea hadi Mei 11.

Hali ya dharura pia ilikuwa imetekelezwa mara mbili hapo awali katika mikoa tofauti ya Japani, kati ya mwezi Aprili 2020 na Januari 2021.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad