Jiji la Beijing laipiku New York, laongoza kwa mabilionea wengi zaidi duniani



Beijing sasa ni makao ya mabilionea wengi zaidi kuliko miji mingine yoyote duniani, kwa mujibu wa wa orodha ya hivi punde ya Forbe ya watu tajiri.



Mji huo mkuu wa China uliongeza mabilionea 33 mwaka uliopita sasa una mabilionea 100, lilisema gazeti hilo la biashara.

Uliushi kwa karibu mji wa New York, ulio na mabilionea 99 na ambao umekuwa ukiongoza orodhaa hiyo kwa miaka saba mtawalio.

Juhudi za haraka za China kudhibiti ugonjwa wa Covid-19, kupanda ngazi kwa mashirika yake ya kiteknolojia na masoko ya hisa kuliisaidia kupata nafasi hiyo ya kwanza.

Ingawa Beijing sasa ina mabilionea zaidi ya Big Apple, thamani jumla ya mabilionea wa Jiji la New York walisalia kuwa dola bilioni 80 sawa na(Pauni bilioni 58) za Marekani ambayo ni ya juu zaidi kuliko ile ya wenzao wa Beijing.

Mkazi tajiri zaidi wa wa Beijing ni Zhang Yiming, mwanzilishi wa programu tumishi ya kushirikisha video -TikTok na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni mama ya ByteDance. Thamani ya utajiri wake iliongezek amara mbili hadi dola bilioni 35.6.

Tofauti na mwenzake, mkazi tajiri zaidi wa New York, Meya wa zamani wa Michael Bloomberg, aliye na utajiri wa thamani ya dola bilioni 59.

Mchango wa biashara ya mtandaoni China

China na Marekani zimeshuhudia kukua na kuimarika kwa kampuni zao teknolojiawakati wa janga la corona kwani watu zaidi walianza kununua bidhaa mitandaoni na kutafuta vyanzo vya burudani.

Hali hii ilichangi aukuaji wa mali binafsi ya wamiliki na wenye hisa wa kampuni hizo kubwa za teknolojia.

Bezoz
China, ambayo Forbes ilijumuisha Hong Kong na Macau katika hesabu zake, ilichagia kuongeza mabilionea zaidi katika orodha yake kuliko nchi nyengine yoyote duniani, ikiwa na matajiri wapya 210.

Nusu ya mabilionea wapya wa China walipata utajiri wao katika biashara ya utengenezaji au teknolojia, na sasa orodha hiyo inamjumuisha bilionea mwanamke Kate Wang ambaye alipata utajiri wake kutokana na e-cigarettes.

Ikiwa na jumla ya mabilionea 698, inakaribia Marekani, ambayo bado inaongoza kwa kuwa na mabilionea 724.

Bilionea mmoja kila baada ya saa 17
India ilikuwa ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya mabilionea, ikiwa na mabilionia 140. Kwa jumla, kulikuwa na mabilionea 1,149 kutoka Asia ya Pasifiki wenye jumla ya utajiri wa dola trilioni 4.7, ikilinganishwa na Marekani yenye mabilionea wenye jumla ya thamani ya utajiri kiasi cha dola trilioni 4.4.

Jeff Bezos, mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Amazon, amesalia kuwa mtu tajiri zaidi duniani kwa miaka minne mfululizo. Utajiri wake umekuwa kwa dola bilioni 64 zaidi na kufikia dola bilioni 177 mwaka jana.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad