Kampuni Lesotho Yaruhusiwa Kuuza Bidhaa za Bangi Ulaya





Kampuni yenye makao yake nchini Lesotho imeruhusiwa kukuuza mazao ya bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.

 

 

Kampuni hiyo kwa jina, MG Health, imesema Alhamisi kwamba imepokea uthibitisho rasmi kwamba mchakato wake wa utengenezaji unakidhi viwango vya uzalishaji vya Muungano wa Ulaya.

 

 

Kampuni hiyo inakuwa ya kwanza barani Afrika kuuza bangi kwa ajili ya dawa kwa Muungano wa Ulaya.

 

 

“Kile ambacho hii inamaanisha ni kwamba tuna idhini ya kuuza bidhaa zetu kama API [ kiungo cha kifamasia] ndani ya Ujerumani, na soko pana la Muungano wa Ulaya . Tunatarajia kuanza mwezi Juni ,” Shirika la habari la Reuters lilimnukuu Mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Andre Bothma akisema.

 

 

Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuhalalisha kisheria kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa mwaka 2017.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad