Kifahamu kikosi cha Afrika LaLiga All Star



Kwa miaka mingi Afrika imekuwa ikizalisha wachezaji mbalimbali maarufu ambao wamekuwa wakifanya makubwa katika Ligi Kuu  ya Hispania LaLiga pamoja na kuyawakilisha vema mataifa yao.



Wachezaji hao ni kuanzia magolikipa, mabeki imara, viungo hadi safu ya washambuliaji kama vile ambapo hapa tutawaangazia nyota 18 waliyopata bahati ya kucheza Laliga huko nyuma na hata wa sasa ambao wanatupatia LaLiga All Star African dream team.

Legendary, Carlos Kameni



Mlindalango raia wa Cameroon, Carlos Kameni ambaye amepata kutumia muda wake mwingi wa soka la kulipwa Nchini Hispania kwenye klabu ya Espanyol, amecheza michezo 200 kwenye misimu yake nane LaLiga. Baadae alikwenda Ufaransa na Uturuki, alianza kuitumikia nchi yake akiwa na miaka 17  kwenye mechi dhidi ya Indomitable Lions lakini pia michuano ya World Cup mara mbili na Africa Cup of Nations mara sita.

Beki kisiki Allan Nyom

Huyu ni mzaliwa wa Ufaransa, aliyepata nafasi ya kuitumikia Cameroonian tangu mwaka 2011. Kwa sasa anaitumikia Getafe, muda mwingi ameutumia akiwa na Granada, amecheza jumla ya mechi 220 kwenye misimu yake sita ndani ya klabu, akiwa Getafe Nyom alikuwa moja kati ya wachezaji wakutumainiwa.



Djené Dakonam

Maarufu kama Djené, Djené Dakonam ni raia wa Togo ambaye anakipiga Hispania kwenye klabu ya Getafe CF akiwa kama nahodha na timu yake ya taifa ya Togo. Alipokuwa Coton Sport, Cameroonian Elite On, Djené alikwenda kwa majaribio LaLiga SmartBank na kujiunga na AD Alcorcón. Lakini kwa sasa beki huyo wa kati anakipiga Getafe CF.



Joseph Aidoo
Alitengeneza jina kubwa pale Ghana mpaka kutwaa tuzo ya beki bora wa ligi mwaka 2014, kisha baadaye kujitengenezea jina lake barani Ulaya, Swiden klabu ya Hammarby kisha Ubelgiji kwenye timu ya Genk na kujiunga na RC Celta mwaka 2019, akishiriki michezo 50.

Kiungo mnyumbulikaji Samuel Chukwueze

Kinda wa miaka 21 amekuwa kivutio pale Villarreal CF akiwa amejiunga mwaka 2017 akiwa na miaka 18 na msimu uliyopita amefanya makubwa akiwa ametokea kwenye michezo 100 mwaka huu kwenye michuano yote huku wakimfananisha aina yake ya uchezaji na Arjen Robben.



Yaya Touré
Ni moja kati ya wachezaji bora kabisa Barani Afrika wa muda wote. Kiungo huyo ameyafurahia zaidi maisha yake ya soka alipokuwa Hispania pale LaLiga alipokuwa akiitumikia FC Barcelona kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 akiwa amecheza michezo 74, magoli manne kabla ya kumtimkia Premier League.

Akiwa Ivory Coast uwezo wake ulianza kuonekana miaka ya 2006, 2010 na 2014 FIFA World Cups. Akifunga jumla ya magoli 19 kwenye michezo 101 aliyotumikia timu yake ya taifa,



Mouhamadou Diarra

Nyota wa Mali aliyeanzia soka lake akiwa na miaka 17 pale Greek club OFI,  Vitesse Ubelgiji, Lyon akishinda taji moja kwenye misimu yake miwili. Na kusaini Real Madrid kwa euro milioni 26, katika msimu wake wa 2006–07 , Diarra alikuwa wachezaji muhimu wa Fabio Capello. Ameonekana kwenye michezo 33 kati ya 38 ndani ya Madrid akishinda mara tatu, akishinda mataji mawili ya LaLiga (2007, 2008) kabla baadaye kwenda kucheza Monaco na Fulham.



Geoffrey Kondogbia
Akizaliwa Ufaransa, Kondogbia akianza maisha yake ya soka Lens kisha Sevilla akiwa na umri wa miaka 19. Miaka miwili baadaye Ufaransa kisha Italy na kurudi Hispania ndani ya klabu ya Valencia kwa mkopo kisha moja kwa moja mwaka 2018. Kisha kujiunga na  Atleti kwa mkataba wa miaka minne mwaka 2020.

Samuel Eto’o
Mshambuliaji hatari aliyewahikutokea Afrika kwa miongo kadhaa. Samuel Eto’o alianzia Real Madrid akiwa na miaka 16. Mwaka 1999 akajiunga na RCD Mallorca kisha RCD Espanyol na CD Leganes kisha kufunga goli 54 kwenye michezo yake 133 kwenye misimu mitano.

Ametumikia FC Barcelona kuanzia mwaka 2004 hadi 2009, akifunga magoli 108 kwenye mechi 144 alizocheza. Eto’oa amefurahia maisha yake ya soka la kimataifa akibeba vikombe 118 na akiwa amefunga magoli 56.

Youssef En-Nesyri
Mmorocco, Youssef En-Nesyri ametengeneza jina lake ndani ya miaka mitano. En-Nesyri ametumia maisha yake ya soka Hspania akiiwakilisha Málaga, Leganés na Sevilla.

Akiwa na miaka 23 ameiwakilisha nchi yake mara 37 na kufunga magoli 11. Kwa sasa ni moto wa kuotea mbali pale Sevilla, akiwa amefunga magoli 17 katika michezo yake 33 msimu huu.

Fredi Kanouté
Kanouté ni mzaliwa wa Ufaransa lakini asili yake ni nchini Mali ambaye amliwahi kushinda mchezaji bora wa mwaka Afrika 2007, mbali na hilo ana mataji mengine mengi tu mawili ya UEFA Cups, Copa del Reys mawili, UEFA Super Cup moja na Spanish Super Cup moja, Kanouté amefanya makubwa Ulaya na kuhitimisha safari yake akiwa icon pale Sevilla, michezo 209 akifunga magoli 89. Akitundika daluga katika timu yake ya taifa mwaka 2010, akiifungia goli 23 kwenye mechi 39.

Wilfred Agbonavbare (Kipa, Rayo Vallecano); Thomas N’Kono (kipa, RCD Espanyol); Samuel Umtiti (beki, FC Barcelona); André-Frank Zambo Anguissa (kiungo mkabaji, Villarreal CF); Pape Kouli Diop (kiungo mkabaji, SD Eibar); Paul Akouokou (kiungo wa kati, Real Betis) na Ansu Fati (mshambuliaji, FC Barcelona).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad