Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA imesema Kimbunga JOBO kimepunguza kasi mara baada ya kuingia kwenye mazingira ya upepo kinzani hivyo kwasasa kimbunga hicho ni hafifu.
“Kwa sasa Kimbunga Jobo ni kimbunga hafifu kinachosafiri kwa kasi ya kilometa 18 kwa saa Baharini, hata hivyo kitasababisha mvua kubwa katika maeneo machache ya Ukanda wa Pwani leo na kesho na upepo huo utasababisha mawimbi makubwa Baharini”