Licha ya wamiliki wa klabu ya Manchester United kuomba radhi siku chache zilizopita baada ya kukubali kushiriki kwenye michuano mipya ya European Super Ligi , lakini mamia ya mashabiki wa klabu hiyo wameandama jioni ya leo Aprili 24, 2021 kuutaka uongozi huo uachie ngazi.
Mashabiki hao wameandamana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza unaosomeka “Glazers Out. Edwoord ward Out” ukiwa na tafsiri ya kutaka wamiliki wao waachie ngazi pamoja na makamu mwenyekiti mtendaji Edwoord ward ajiengue.
Mgomo huo umekuja siku tatu baada ya klabu hiyo kutangaza kujitoa kwenye michuano hiyo mpya na wamiliki hao kuomba radhi kwa mashabiki kupitia vyanzo mbalimbali vya habari lakini mashabiki hao hawaoonekani kuridhishwa na namna klabu hiyo inavyoendeshwa.
Ikumbukwe kuwa, Jumapili ya Aprili 18, 2021 waandaaji wa michuano hiyo mipya kwa kushirikiana na benki ya Street Bank JP Morgan, waliorodhesha vilabu 12 vilivyothibtisha kushiriki mihchuano hiyo na klabu ya Manchester United ikiwemo.
Mashabiki hao mbali na kuwapinga wamiliki wa klabu hiyo, lakini wanapinga klabu yao kushiriki kwenye michuano hiyo kwasababu itaondoa msisimko na kuondoa mahusiano ya mashabiki na klabu yao hiyo.