Kocha Yanga Aibuka na Mikakati Mipya




KATIKA kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la FA, Kocha wa Makipa wa Yanga raia wa Kenya, Razack Siwa, amesema wataingia uwanjani kucheza michezo hiyo kama fainali ili kufanikisha malengo yao ya kutwaa ubingwa.

 

Hiyo ikiwa siku chache katika kuelekea mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano hiyo utakaopigwa kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa dhidi ya Prisons.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Siwa alisema licha ya kuupambania ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini nguvu zao hivi sasa wanazielekeza katika michezo ya FA kwa lengo la kubeba kombe hilo.



Siwa alisema katika michezo iliyobaki ya ligi na FA, watahakikisha wanacheza kama fainali ili kufanikisha malengo waliyojiwekea msimu huu ya kubeba ubingwa.

 

Aliongeza kuwa, anaamini haitakuwa kazi nyepesi, lakini watahakikisha wanapambana kwa kushirikiana na wachezaji, viongozi na mashabiki ambao ndiyo watu muhimu kwao.



“Tumepoteza mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Azam, lakini haitatufanya tushindwe kufanya vema katika mchezo wetu wa FA dhidi ya Prisons.

 

“Tumeona makosa yaliyosababisha sisi tupoteze, niahidi kufanyia marekebisho kwa ajili ya kukiboresha kikosi chetu ili yasijitokeze tena.“Mchezo uliopita kipa wetu Shikalo (Farouk) alitupiwa lawama kutokana na aina ya bao tulilofungwa, hivyo niahidi kulifanyia kazi ili lisijirudie,” alisema Siwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad