Korea Kaskazini yaripoti kwa WHO kuwa Hakuna corona nchini humo





Korea Kaskazini imeripoti kwa Shirika la Afya Ulimwenguni kuwa hakuna kesi ya corona nchini humo.
Maafisa wa Korea Kaskazini, walitangaza katika ripoti ya hivi karibuni iliyowasilishwa kwa WHO kwamba hakuna mtu yoyote mwenye virusi vya corona nchini humo.

Mwakilishi wa WHO wa Korea Kaskazini Edwin Salvador alisema kuwa jumla ya watu 23,121 walipimwa kote nchini tangu kuanza kwa janga hilo.

Watu 732 kati yao walipimwa katika kipindi cha Machi 26 hadi Aprili 1 na hakuna aliyekutwa na virusi vya corona.

Korea Kaskazini ilitangaza jana kuwa haitashiriki Olimpiki ya Tokyo ili  kulinda wanariadha dhidi ya janga la corona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad