Majaliwa Asisitiza: Dodoma ni Makao Makuu



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewatoa hofu Watanzania waliofikiri mkakati wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi hautoendelea.

 

 

Akihutubia Bungeni Dodoma leo Ijumaa, Aprili 16, 2021, Majaliwa amesema, “Serikali imeweka mfumo mzuri wa kuhakikisha Makao Makuu ya Nchi yanaendelezwa kwa kujenga na kuendelea na mipango ya maendeleo ya Jiji la Dodoma.

 

 

Ameongeza, “Watumishi wapo Dodoma, shughuli zote za Serikali zinafanywa, ujenzi wa miundombinu mbalimbali unaendelea. Niwahakikishie Watanzania Dodoma inaendelea vizuri”

 

 

 

“Hatua mbalimbali za utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais zimeanza kuchukuliwa ikiwemo kuandaa muundo wa wizara yenyewe, kupitia sera ya uwekezaji upya ya 1996 na sheria ya uwekezaji 1997 ili kubainisha maeneo yenye uhitaji wa maboresho.

 

 

“Nitumie fursa hii kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa uamuzi wa kurejesha jukumu la uwekezaji katika Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ni ishara ya wazi kuwa na imani kubwa aliyonayo kwa ofisi ya WaziriMkuu
nami namhakikishia kuwa sitamuangusha.

 

 

“Natoa melekezo kwa wizara na taasisi zote zinazowahudumia wawekezaji kuhakikisha wanawezesha uwekezaji katika maeneo yao kwa kutoa huduma stahiki na kuhakikisha taarifa muhimu zinapatikana kwa wakati na kuondoa usumbufu.

 

 

“Nasisitiza watendaji wajiepushe na uombaji wa rushwa , urasimu usiokuwa wa lazima katika kuwahudumia wawekezaji ili kujenga imani baina ya sekta ya umma na sekta binafsi ili tuweze kuzungumza lugha moja,” Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad