Majani Umeteleza Kumshambulia Binti yako Kwenye Radio, Wewe ni Sehemu ya Tatizo

 


Majani anasema mtoto wake alimkataa, ila hasemi ilikuwaje wakafika hali hiyo.


Majani anasema kwenye radio kuwa mtoto wake kazaliwa na mama asiyestahili.


Majani anaitangazia dunia kwamba binti yake amelaanika.


Kwa mtu mwenye hekma na utulivu wa akili utagundua Baba pia ana tatizo kubwa kuliko mama anaetupiwa lawama zote.


Majani alishindwa kusimama kama baba wakati wa makuzi ya Paula leo unakuja kuutangazia umma kwamba damu yako imeshindikana.


Majani umeteleza ni heri ungeendelea kukaa kimya tunge assume una busara.


Ona sasa unalaumu binti yako na mama yake wanapeleka vitu mitandaoni, na wewe unafanya kile kile unatumia media kutoa hukumu kwa damu yako.


Siku Paula akirudi kwenye media kutolea ufafanuzi kauli zako utasema amekukosea heshima wakati umeendelea kumchafua??


Majani unaumizwa na mtoto wako kuvujisha videos, lakini uhoni tatizo la baba yake wa kufikia kumtongoza na kumtumia dudu analoliona mama yake. Majani uhoni kama ingekuwa fedhea sana kwako kama bwana angefanikiwa kuwala baby mama wako na binti yako?


Majani tumia busara kama baba, linapofika suala la binti yako wewe sio majani wewe ni baba. Kamwe baba huwa hasimami kuishambulia damu yake ni heri ungeendelea kukaa kimya.

JF

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad