Mama Ataka Uchunguzi Kifo cha Mwanaye


KABURI la mtoto Abdul Bakari (9) lililofukuliwa eneo la Kaloleni wilayani Kiteto mkoani Manyara chini ya ulizi mkali wa jeshi la Polisi limezua maswali mengi na taharuki wa wananchi.


Marehemu Abdul Bakari alizikwa Aprili mosi mwaka huu makaburi ya mtaa wa Kaloleni wilayani Kiteto, kufuatia kifo chake katika hospitali ya wilaya ya Kiteto alipokuwa amelazwa.

Taarifa za ndugu na jamàa wa marehemu zinaeleza kuwa mtoto huyo alilazwa kwa siku kadhaa katika hospitali hiyo akitibiwa tatizo la kupungua damu.

Wakati mtoto huyo anauguzwa mama yake mzazi hakuwepo kwani walitengana na baba yake kutokana na matatizo ya kifamilia ambapo baada ya kifo hicho alijulishwa.


Mama mzazi aliomba mwanae asizikwe mpaka afike na kufanya jitihada siku hiyo kwani alifariki usiku na asubuhi ya saa tatu mama alikwishafika lakini alijuta kwani mwanae alikuwa ameshazikwa.


Utata ulianzia hapo kisha kuomba taratibu za kisheria mwili ufukuliwe ili uchunguzwe sababu za kifo chake kwani alipata hofu kuwa kwanini azikwe haraka kiasi hicho.


Hata hivyo, mwili huo ulifukuliwa chini ya ulinzi mkali akiwepo daktari kufanya uchunguzi kisha walifukia na taratibu za kisheria zinaendelea.


Aidha, baadhi ya majirani akiwemo Halida Fumito aliekeza kuwa ameshangazwa na matukio ya baba wa marehemu Bakari toka siku ya mazishi.


Alisema siku ya mazishi alionekana ‘front’ kutaka kubandika maji ya kuosha maiti mwenyewe ndipo majirani wakamsihi awaachie wafanye wenyewe.


“Tulimwambia asubiri tumsaidie, tukawasha jiko na kubandika maji lakini alitaka abandike mwenyewe jambo ambalo sio la kawaida”

Hata hivyo, baada ya uchunguzi taratibu za kufunguliwa kesi zinaendelea kwani anayefungua ni mama mzazi kutaka kujua kilichomuua mwanae.


STORI: MOHAMED HAMAD, MANYARA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad