Joseph Magufuli ambaye ni mtoto wa aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli amesema mama yake, Janet anaendelea na matibabu baada ya kupata mshtuko kufuatia kifo cha mumewe.
Akizungumza kwa niaba ya familia ya Magufuli wakati wa kongamano la viongozi wa dini, Joseph amesema mama yake hayupo vizuri kiafya lakini anaendelea na matibabu.
“Mama hakuweza kuja kwa sababu ya tatizo la kiafya alipatwa na mshtuko baada ya baba kufariki, yupo anaendelea na matibabu.”
“Mama anawashukuru viongozi wa dini na watu wote kwa kuliombea Taifa wakati wote wa msiba na ilikuwa jambo gumu kumpoteza mzazi na kiongozi wa Taifa,” amesema.
Joseph amewasisitiza Watanzania kuendelea kumuomba Mungu ili upendo, amani na mshikamano viendelee kutawala nchini.