Marufuku kuripoti mgogoro kwenye kasri la Mfalme, Jordan




Jordan imedhamiria leo kuufunika mgogoro uliotokea katika kasri la Mfalme wa nchi hiyo kwa kuviamuru vyombo vyake vya habari kukoma kuripoti kuhusu madai ya njama ambayo serikali imesema inamhusisha kaka ya Mfalme Abdullah II.

Jordan orders media ban, reframes 'wicked plot' as family feud | The Times  of Israel

Mwanamfalme Hamzah Jumamosi aliwakosoa vikali viongozi wa Jordan kuhusu kile alichosema ni kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani – lakini mara ghafla akabadilisha jana kauli hiyo kwa kuahidi kuwa mtiifu kwa familia ya Kifalme.

Mwendesha mashitaka wa serikali amepiga marufuku uchapishwaji wa habari kuhusu uchunguzi kuhusu kile serikali ilisema ni njama ovu dhidi ya Jordan inayoyahusisha makundi ya kigeni.

Serikali imemtuhumu Hamzah – mwanamfalme aliyezuiwa kuwa mrithi wa kiti cha Ufalme mwaka wa 2004 – kwa kuhusika na njama ya kuyumbisha uthabiti wa usalama wa taifa hilo la Kifalme na pia ikawakatama karibu watu 16.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad