Matendo ya chuki kwa raia wa Marekani wenye asili ya Asia yaongezeka





Wimbi la matendo ya chuki kwa watu wa asili ya Asia nchini Marekani ambalo lililotokana na janga la virusi vya corona mwaka jana, limeendelea mpaka mwaka huu. Takwimu za idara ya polisi zinaonyesha miji 15 mikubwa ya Marekani, imeripoti kuongezeka kwa asilimia 169 kwa ghasia dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Asia. Robo ya kwanza ya mwaka huu imekuwa na visa vingi ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana. Kuongezeka huko kwa kasi kunafuatia kuongezeka kwa karibu asilimia 150 mwaka jana kwa kufanyiwa uchambuzi, na kuja kwa utawala wa sasa wa rais Joe Biden. Utawala wa sasa umedhamiria kupitisha sheria itakayo iwezesha wizara ya sheria kuwa na idara itakayo shughulikia masuala hayo. Katika majiji ya New York, Los Angeles na miji 13 mingine, polisi imechunguza jumla ya mashambulizi 86 ya Wamarekani wenye asili ya Asia katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Hilo ni ongezeko kwa matukio 32 ikilinganishwa na kipindi hicho kwa mwaka jana 2020.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad