Mbowe adai kubambikwa kodi ya Sh2 bilioni, TRA yamtaka awapelekee malalamiko yake




 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe ametaja sababu ya kuamua kuondoka nchini na kwenda kuwekeza nchi zingine kuwa ni tozo ya kodi kiasi cha Sh2 bilioni aliyopewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


Hata hivyo, Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa kodi na mawasiliano, Richard Kayombo alipoulizwa kwa simu leo, amesema masuala ya kodi ni kati ya mlipa kodi na mamlaka hiyo, hivyo hatayazungumza kwenye vyombo vya habari.  


"Sipendi kuongea kwenye hilo kwa sababu suala la mlipa kodi anawasiliana na sisi moja kwa moja. Mlipakodi kama ana concern (jambo) anayo haki ya kuwasilisha lalamiko lake katika ngazi mbali mbali za Mamlaka au katika vyombo vya usuluhishi wa migogoro ya kodi,” amesema Kayombo. 


Mbowe ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 11, 2021 wakati akilihutubia Taifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, akidai kuwa kabla ya kupewa tozo hiyo aliondolewa dhamana katika kesi yake ya uchaguzi na kuwekwa ndani miezi minne na kipindi hicho TRA walimtumia barua pepe kuelezea deni hilo la kodi wakijua fika hakuwa katika nafasi ya kupata ujumbe huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad