Mbunge Akamatwa na Polisi, Wabunge Wacharuka, Spika Aahirisha Kikao






SPIKA wa Bunge la Kenya (Senate), Ken Lusaka amelazimika kuahirisha kikao vya bunge kwa muda, kufuatia kukamatwa kwa Mbunge wa Meru, Franklin Mithika Linturi leo asubuhi akielekea bungeni.

 

Linturi amekamatwa na maafisa wa polisi mara tu baada ya kutua viwanja vya bunge kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha.

 

Wakati kikao cha bunge kikiendelea, Spika aliulizwa kama Polisi waliomba ruhusa kwake kabla ya kumkamata Linturi lakini akasema hajatoa kibali. Hapo ndipo wabunge walipocharuka na kutaka kikao cha bunge kiahirishwe mara moja hadi mwenzao atakapoachiwa.

 

“Mheshimiwa Spika hatuwezi kujiona tupo salama hapa ndani kama mmoja wetu hayupo salama” amedai Seneta wa Kisumu Fredrick Otieno.

 

“Mheshimiwa Spika napenda kujua polisi wanapata wapi mamlaka ya kuja hadi kwenye viwanja vya bunge na kumkamata mbunge bila idhini yako. Hii ni dharau,” amehoji Samson Cherarkey, Seneta wa Nandi.

 

Kufuatia malumbano hayo, Spika amelazimika kuahirisha kikao hadi watakapojua hatma ya mwenzao. Katiba ya Kenya inazuia Mbunge (Senetor) kukamatwa au kuhojiwa na chombo chochote cha usalama bila ruhusa ya Spika.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad