Mbunifu wa Marekani aliyetumia picha ya msikiti wa kihistoria uliopo pwani ya Kenya, Lamu katika fulana aliyoivaa nyota wa Marekani Jay-Z aomba radhi.
Viongozi wa msikiti wa Riyadha walioghadhabishwa na kupinga kwa fulana yenye msikiti wa Lamu kuvaliwa na msanii HUYO kwa kuhofia kuvaliwa katika sehemu za starehe wameridhia maombi ya msamaha wa mbunifu huyo.
“Tumekubali msamaha wake kwa kuwa alifanya kwa nia njema,” maofisa wa msikiti wamesema.
Mbunifu Zeddie Loky aliripotiwa kutengeneza fulana hiyo ili kuutangaza mji wa Lamu.
Lamu imetajwa na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO-kuwa eneo la urithi wa dunia na msikiti huo uliojengwa karne ya 19 ni miongoni mwa vivutio vikubwa.
Ni msikiti ulioanza tangu mwaka 1837, ni miongoni mwa taasisi za zamani zaidi za ufundishaji za Kiislamu katika Afrika Mashariki.
Waumini walipata ghadhabu walipoona picha ya mwanamuziki wa Marekani akiwa amevaa fulana yenye picha ya msikiti wa Lamu katika makundi ya WhatsApp , alisema katibu mkuu wa msikiti huo bwana Abubakar Badawy.