Mdee Acharuka: Serikali Ilipe Deni




Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, ameitaka Serikali kulipa deni inalodaiwa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii ili Wastaafu walipwe kwa wakati.

 

Akiwa Bungeni leo, Mdee amesema Duniani kote Mifuko ya Jamii huisaidia Serikali kufanya shughuli za maendeleo kwa kukopa kwa riba na kulipa, lakini kwa Tanzania Serikali na Taasisi zake zinakopa kwa riba lakini hazilipi.

 

Amebainisha kuwa, Hotuba ya Waziri Mkuu inaonesha kuunganishwa kwa Mifuko mwaka 2018 kumeongeza ufanisi, ubora na kupunguza gharama za uendeshaji.

 

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) inaonesha Deni la Serikali ni Tsh. Trilioni 2.7 lakini haijajumuisha Tsh. Trilioni 1.7 za PSSF.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad