"Mimi ni Mzuri Sana Nikipendeza Nitachukua Wanaume wa Watu Sana" - Chemical

 


Rapa Chemical amesema yeye ni mwanamke mzuri na ameumbika vyema hivyo akiamua kupendeza anaweza akawaiba wanaume au atawachukua wanaume wengi ambao tayari wana wapenzi wao.

Pia Chemical amesema watu wasiuchukulie poa muoenekano wake kisa anafanya muziki wa HipHop kwani akisema ajipodoe au apendeze kama wanavyofanya wanawake wengine basi atawachukulia mabwana zao.

"Nikiamua kuvaa nitachukua mabwana wengi sana ndiyo maana sitaki kukaa huko, mimi ni mzuri sana na nimeumbika kila kitu siku nikiamua kujipodoa kama wanavyofanya wengine au wanavyovaa mtanipiga kwa sababu nitachukua vitu vyenu vingi na sipo tayari kugombana na watu" ameeleza Chemical 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad