Msomi UDSM ashauri uhakiki majina kwa wanaoteuliwa






Saa chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Thobias Mwesiga Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ameshauri kabla ya majina ya walioteuliwa hayajatangazwa yahakikiwe, ili kuondoa mkanganyiko.


Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwesiga ikiwa chini ya saa 24 tangu kuteuliwa kwake.



Jana April 4, 2021, saa 4 usiku Rais Samia alimteua Mwesiga kuwa ni miongoni mwa wakuu wa mashirika aliowateua, lakini leo asubuhi ametengua uteuzi huo na kumrejesha Dk James Mataragio kuendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC.



Akizungumza na Mwananchi leo Aprili 5, 2021, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Faraja Kristomus amesema ni vema kabla majina ya watu hayatangazwa ufanyike uchambuzi wa kina.



“Ofisi ya Rais ni taasisi, hivyo inawezekana kuna baadhi ya taarifa za ziada kuhusu huyo mtu Rais hakuwa nazo, lakini baada ya kupata taarifa hizo ndio akaamua kufanya uamuzi huo,” amesema na kuongeza:



“Wakati mwingine kuna watu walimpenyezea jina au inawezekana pia hakuwa amenuia kumtengua Mataragio ilitokea kwa bahati mbaya,” amesema.



Hata hivyo, amewashauri wasaidizi wa Rais kuhakikisha kabla majina ya walioteuliwa hayajatangazwa wajihakikishie vizuri, ili kuondoa mkanganyiko.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad