JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa kikosi cha Yanga amesema kuwa kitu kikubwa ambacho anakitazama kwa ajili ya mchezaji atakayeanza kikosi cha kwanza ni kujituma mazoezini pamoja na nidhamu kiujumla.
Mwambusi amekabidhiwa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7, kwa kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovu wa vinara hao wa ligi wakiwa na pointi zao 50.
Akizungumza na Championi Jumatano, alisema kuwa kila mchezaji ana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwa sababu wachezaji wake wote ni sawa na wapenda kile ambacho wanakifanya.
“Kwa upande wa maandalizi ninaona kwamba kila kitu kinakwenda sawa. Ili kupata namba kikosi cha kwanza ni lazima mchezaji awe na juhudi mazoezini pamoja na nidhamu, hakuna mwenye uhakika wa namba kwa sasa,” alisema Mwambusi.
Mchezo wao ujao kwenye ligi kwa Yanga ni dhidi ya KMC iliyo nafasi ya tano na pointi 35 utachezwa Uwanja wa Mkapa, mchezo wa mzunguko wa kwanza, ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga.