Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Lupembe na wanachama 150 watimkia CCM




MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Lupembe mkoani Njombe Enocent Gwivaha pamoja na wanachama 150,wamehama Chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao wapya wamepokelewa na kukabidhiwa kadi za uanachama na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya katika mkutano wa mbunge uliofanyika eneo barazani kata ya Lupembe wilayani Njombe.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wengine mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Chama cha Mapinduzi,aliyekuwa mwenyekiti huyo wa Chadema amesema kuhama kwao ni maamuzi binafsi waliiyokuwa nayo ili kuungana na mamilioni ya watanzania walio kwenye Chama cha Mapinduzi.

“Kuhama ni maamuzi yetu sahihi baada ya kuona ni vema tukaungana na mamilioni ya watanzania kwa ajili ya kuendeleza taifa letu,tunashukuru sana viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa kutupokea”alisema Enocent

Wameahidi kuwa waaminifu katika kukitumika Chama cha Mapinduzi “Tutakuwa wanachama waaminifu,tutafanya kazi ya Chama mahali popote mtakapotutuma na tupo tayari tayari kuungana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wetu.Najua kwamba kuna watu pengine wanaumia sana kwasababu mimi nilikuwa kiongozi wao wa jimbo lakini pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema taifa,watu watatoa kejeli lakini haya ni maamuzi binafsi ambayo tumeamua naomba myaheshimu”aliongeza Gwivaha

Hitla Msola ni katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Njombe na Betrece Malekela ni mwenyekiti wa jumuiya ya wananawake wa CCM wilaya hiyo ni miongoni mwa viongozi waliowapokea wanachama hao wamekiri kupokea wanachama hao huku wakishuhudia usumbufu waliokuwa wakiupata jimboni hapo kupitia viongozi hao huku wakiamini sasa kuwa pamoja katika maendeleo ya Lupembe.

“Bwana Enocent alitusumbua sana hasa kipindi cha uchaguzi na wakati mwingine tulishindwa hata kurudi majumbani mwetu kwaababu yake”alisema Msola

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swale amewapongeza wanachama hao wapya kujiunga na Chama cha Mapinduzi na kuahidi kushirikiana nao katika maswala ya maendeleo ya jimbo la Lupembe.
 
Baadhi ya wanachama wapya kutoka Chadema wakila kiapo mbele ya wananchi mara baada ya kuhama Chama hicho na kujiunga na Chama cha Mpainduzi.
 
Mbunge wa jimbo la Lupembe akimkaribisha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema jimbo la Lupembe mara baada ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi
 
Wanachama wapya na baadhi ya wananchi wakipongezana baada zoezi la kupokea wanachama wapya kukamilika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad