Ndege ya kijeshi ya operesheni dhidi ya shirika la kigaidi la Boko Haram imetoweka kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Umma na Habari wa Jeshi la Anga la Nigeria Edward Gabkwet, alitangaza katika taarifa kwamba ndege ya jeshi iliyotumwa kwenye operesheni inayoendelea dhidi ya Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi, imetoweka katika jimbo la Borno.
Gabkwet alisema, "Mawasiliano na ndege hiyo yalikatizwa mwendo wa saa 17.08 (majira ya eneo hiyo) jioni ya Machi 31."
Baada ya tukio hilo, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Nigeria Jenerali Oladayo Amao alitembelea mkoa huo.
Amao alisema kuwa shughuli ya utafutaji wa ndege hiyo inaendelea na kwamba wameazimia kuhakikisha amani inadumishwa katika maeneo ya kaskazini mashariki.
Wanajeshi 7 walifariki nchini Nigeria mnamo tarehe 21 Februari wakati ndege iliyokuwa imebeba wanajeshi ilipoanguka katika mji mkuu wa Abuja.
Zaidi ya watu 20,000 wamepoteza maisha katika mashambulizi ya kigaidi yaliyoendeshwa na Boko Haram tangu mwaka 2009 nchini humo.
Shirika hilo la kigaidi pia limefanya mashambulizi katika maeneo ya mipaka ya nchi jirani kama vile Cameroon, Chad na Niger tangu mwaka 2015. Watu wasiopungua 2,000 walifariki kwenye mashambulizi yaliyoendeshwa na shirika la kigaidi katika Bonde la Ziwa Chad.
Mamia ya maelfu ya watu walilazimika kuhama makazi yao nchini humo kutokana na ya kigaidi na mizozo iliyokithiri.