Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Musa Assad, amesema ubadhirifu unaotokea kwenye Wizara huwa hauna maelezo zaidi ya kusema 'Ni maamuzi ya Baraza'
Amesema suala hilo linafanya kuwepo kwa mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya mali za umma, hivyo ni vizuri kuwa na uwazi katika Baraza la Mawaziri
Ametolea mfano Nchi zilizoendelea kama #Dernmark ambapo taarifa zote za Baraza la Mawaziri huwekwa wazi ili Wananchi ili wajue kinachoendelea
Amesisitiza namna bora ya kupambana na rushwa na ubadhirifu katika ofisi za umma ni kuwa na uwazi