Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi mwaka 2015-2020 na msanii Prof Jay amesema anajua Mbunge wa Jimbo la Muheza, Tanga Mwana Fa ana akili nyingi na ameingia kwenye nafasi ya maamuzi hivyo aendeelee kuimbuka sanaa.
Prof Jay ameendelea kusema Mwana Fa ana uandishi mzuri sana kwenye nyimbo zake hivyo amemuomba asiache kufanya hivyo japo anajua ana majukumu mazito ya kutumikia wananchi wa Muheza.
"Najua Mwana Fa ana akili nyingi, ana talent na ni mmoja kati ya wasanii bora wa HipHop wanaoandika vizuri hata yeye pia ana anasema mimi ni msanii wake bora wa HipHop tena wa muda wote"
"Kitu kikuba ambacho namwambia ni kwamba ameingia kwenye nafasi ya maamuzi ila aendelee kukumbuka huku najua ana majukumu makubwa ya kule Muheza, asiache kufanya hiki kitu ambacho alikuwa anakifanya siku zote najua ana majukumu magumu ila aendelee kufanya" ameongeza Prof Jay
Prof Jay, Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr II Sugu na Mwana Fa ni baadhi ya wasanii wa HipHop hapa nchini Tanzania ambao wameweza kuingia kwenye siasa na kutumikia wananchi.