Pweza mwenye hasira amshambulia mwanasayansi akiogelea





Mwanaume mmoja amepigwa na kile anachoeleza kama "pweza mwenye hasira kali" wakati alipokuwa akiogelea katika pwani ya Magharibi mwa Australia.
Katika video ambayo imeenea mitandaoni, pweza huyo anaonekana majini akimshambulia mtaalam wa jiolojia Lance Karlson.Mnyama huyo alimfuata tena baadaye na kumpiga kwenye mkono, kabla ya kuchapa shingo lake na sehemu ya juu ya mgongo wake .

Mtaalamu huyo aliachwa na uvimbe mwekundu kwenye ngozi yake, ambayo Bwana Karlson alisema ulipungua tu baada ya kumwaga kivywaji cha kola juu ya ngozi yake

Mlinzi huyo wa zamani wa Pwani alikiambia kituo cha habari cha Australia 7News kuwa matibabu anayopendelea zaidi ya kuumwa na wanyama wa baharini ni siki, lakini hakuwa nayo wakati huo.Walakini, alisema kwamba anajua chochote chenye tindikali kinaweza kusaidia, na akaamua kujaribu kutumia cola. " ilibainika kwamba inafanya kazi.

"Bw Karlson anasema alikuwa tayari kujitumbukiza majini kuogelea katika hoteli ambayo yeye na familia yake wamekuja likizo huko Geographe Bay alipokiona kiumbe kinachofanana kama aina Fulani ya samaki kumbe baadaye alibaini kiumbe hicho kilikuwa ni pweza Alipogundua hivyo alisonga karibu na binti yake mwenye umri wa miaka miwili ili kuchukua video na ni wakati huo alipopigwa na pweza huyo ." Pweza huyo aliturukia ,kitu ambacho kilitushangaza' Bw Mr Karlson amesema kupitia barua pepe aliyotuma kwa Reuters. Baadaye alirejea majini akiwa pekee yake na pweza huyo akampata na kumshambulia tena

" Miwani yangu ilijaa ukungu maji yakabadilika rangi na nakumbuka nikiwa nimeshtuka na kuchanganyikiwa' alisema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad