Mrithi wa kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman amesema kwamba Marekani ni mshirika wao wa kimkati na kwamba serikali ya Riyadh inatofauti chache na serikali ya sasa ya Joe Biden, ambazo zinazifanyiwa kazi ili kuweza kuzimaliza kabisa.
Mtawala huyo wa kifalme alisema pia Saudi Arabia haiwezi kukubali shinikizo lolote au kuingiliwa masuala yake ya ndani.
Rais Joe Biden, ambea alisema atafanya mazungumzo na mwenzake wa Saudi Arabia Mfalme Salman, amekuwa akichukua msimamo mkali dhidi ya serikali ya taifa hilo, na hasa kuhusu rekodi zake za ukiukaji wa haki za binaadamu na ushiriki wake katika vita vya Yemen, tofauti na mtangulizi wake Donald Trump, aliyekuwa mshirika madhubuti wa Mwanamfalme Mohammed.