Serikali Yasitisha Matumizi ya Vitamin C Kutibu COVID-19




WIZARA ya afya nchini Uganda imesitisha matumizi ya vitamin C katika kutibu virusi vya Covid-19 kutokana na matumizi mabaya ya wagonjwa.

 

Vitamni C ndiyo moja ya dawa zilizokuwa zinatumiwa kWa wagonjwa wa covid-19 nchini Uganda kwa sababu zinasaidia kuendeleza chembe hai nyeupe(White blood cell) kupambana kuondoa virusi.

 

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya afya wanaoshughulika na masuala ya utafiti, wanadai vidonge vya vitamn C vinapatikana kwa urahisi na hivyo watu hutumia kiholela kupita kiasi na kuleta madhara.

 

Daktari Misaki Wanyegera ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kupambana na virusi vya corona katika wizara ya afya nchini Uganda, amesema walichukua hatua ya kuondoa Vitamic C baada ya wagonjwa hospitalini kukutwa wakitumia hovyo vitamin hizo na kusababisha figo kushindwa kufanya kazi kutokana na matumizi mabaya.

 

Kulingana na ushauri wa madaktari, matumizi ya Vitamin C kwa mgonjwa wa mafua ni tembe 2 kila baada ya saa 8, lakini watu wanatumia mara tatu ya hizo. Mwezi Januari kulikuwa na ukosefu wa Vitamin C za Gramu 100 kote nchini humo kutokana na matumizi mabaya.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad