Shirika la Udhibiti wa Dawa la EMA kuchunguza chanjo ya Johnson and Johnson






Shirika la Udhibiti wa Dawa la (EMA) na Wakala wa Umoja wa Ulaya (EU), limeanzisha uchunguzi endapo chanjo ya corona (Covid-19) iliyotengenezwa na kampuni ya dawa ya Marekani ya Johnson and Johnson inasababisha kuzibika kwa mishipa kama matokeo ya tatizo la kuganda kwa damu.
Katika taarifa iliyotolewa na EMA, iliripotiwa kuwa uchunguzi ulianzishwa baada ya ripoti kwamba kulikuwa na visa vya kuzibika kwa mishipa kama matokeo ya tatizo la kuganda kwa damu kwa baadhi ya watu walipewa chanjo ya "Covid-19 Vaccine Janssen", ambayo ilitolewa kwa mfumo wa dozi moja, tofauti na zingine.

Katika taarifa hiyo ambayo ilibainisha kuripotiwa kwa kesi 4 za tatizo la kuganda kwa damu baada ya chanjo hadi sasa, pia ilieleza kuwa moja yao iligundulika wakati wa majaribio ya kliniki na tatu ziligundulika baada ya chanjo kutolewa nchini Marekani (USA).

Katika taarifa hiyo, ilibainika kuwa kesi moja ilisababisha kifo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad