Vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara Simba SC wanashuka dimbani kuwakabili Dodoma Jiji kutoka makao makuu ya nchi Dodoma, mchezo utakao chezwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar es salaam majira ya Sa 1:00 Usiku.
Simba ndio vinara wa Ligi hiyo kwa alama 58 baada ya kucheza mechi 24, wakiwa wanaongoza kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Yanga wenye alama 57 ambao wapo nafasi ya pili.
Wekundu wa msimbazi watakuwa wakicheza mchezo wa 25 dhidi ya Dodoma jiji ambao wapo katika nafasi ya 6 wakiwa na alama 38 baada ya kucheza michezo 27.
Kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza ambao ulipigwa katika dimba la Jamuhuri Dodoma Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Dodoma Jiji chini ya Kocha Mbwana Makata wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wameshinda mchezo mmoja tu kwenye michezo mitano ya mwisho wakati wenyeji wao hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye michezo mitano ya mwisho, wameshinda minne na sare mchezo mmoja.
Wachezaji Pascal Wawa na Luis Miquiessone wanarejea kwa upande wa kikosi cha Simba baada ya kuukosa mchezo uliopita dhidi ya Gwambina kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano, mchezaji pekee anaekosekana ni Thadeo Lwanga ambaye anamatatizo ya kifamilia baada ya kufiwa na dada yake.
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu utakao pigwa leo ni Gwambina walio nafasi ya 12 wakiwa na alama 30 watakuwa nyumbani kuwakaribisha Mwadui FC wanaoburuza mkia kwenye msimao wa ligi wakiwa nafasi ya 18 na lama zao 16. Mchezo huu utachezwa Saa 10:00 Jioni huku Misungwi Mwanza