TIMU ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu, baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mwadui Fc, kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara mchezo ulichezwa leo Aprili 18, kwenye uwanja Kambarage mkoani Shinyanga.
Goli pekee la Simba limefungwa na nahodha John Bocco dakika ya 66’ aliyeingia kwenye kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo Simba imepaa mpaka nafasi ya pili kwa kufikisha alama 52, ikishuka dimbani mara 21 na Yanga wanaongoza ligi wakiwa na alama 54, baada ya kushuka uwanjani mara 25.