Spika Ndugai atishia kushika Shilingi ya Waziri wa Fedha ikiwa hatakuwa na majibu ya kuridhisha





 Spika wa bunge Job Ndugai amewataka wabunge wa kanda ya Ziwa kuungana kusemea madhara ya zebaki.
Spika amezungumzia fedha zinazotolewa na wahisani kwa ajili ya mapambano ya mazingira akimtahadharisha Waziri wa Fedha kwamba atakamata shilingi ya Waziri hadi ajue kwa nini wanazuia fedha hizo.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati bunge likijadili hotuba ya Wizara ya nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Kauli ya Ndugai ikifuatia mchango wa mbunge wa Viti Maalum Hawa Mchafu ambaye alieleza kuhusu madhara makubwa yatokanayo na zebaki hasa kwa wachimbaji madini.

"Wabunge wa kanda ya ziwa lazima Muungane kulisemea hili, hali siyo nzuri hii zebaki ina madhara makubwa kwa wananchi wetu, siyo jambo la kufumbia macho," amesema Ndugai.

Kuhusu fedha za mazingira amesema kuna ukiritimba kwa Wizara ya fedha ambazo hutolewa kwa ajili ya kupambana na uharibifu wa mazingira akaomba jambo hilo liangalie.

Katika mchango wake Hawa amesema hali ya Afya za wanawake wa kanda ya ziwa hasa wanaofanya Kazi za madini migodini, zimekuwa shakani akaomba Serikali kuingilia kati.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad