Spika Ndugai awaita mawaziri, wabunge bungeni






Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka mawaziri, manaibu wao na wabunge wote wawepo bungeni kesho Alhamisi Aprili 22, 2021 wakati Rais wa awamu ya sita,  Samia Suluhu Hassan atakapolihutubia Bunge.
Rais Samia aliyeapishwa Machi 19, 2021 baada ya kifo cha rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 kesho  atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu awe kiongozi mkuu wa nchi.

Akizungumza leo Jumatano Aprili 21, 2021 Ndugai amesema mbali ya kuwa ni mkutano wa bajeti lakini Bunge hilo lina ugeni mzito wa Rais Samia.

“Kesho tutakuwa na ugeni mkubwa sana hapa Rais wa awamu ya sita anakuja kulihutubia Bunge. Huwezi kujua kesho wala kesho kutwa,  si vizuri kutokuwepo kwenye landmark ya mheshimiwa Rais wa awamu wa sita anapokuja kulihutubia Bunge hili.”

“Wale  mawaziri na manaibu ambao wako huko sijui wapi wote wawepo kesho. Warudi wote wawepo  kesho. Ukumbi utakuwa umejaa wote, gallery zote halafu ndani ya ukumbi wa bunge….haitaeleweka,” amesema.

Amewataka wabunge ambao majirani zao hawapo kuwapigia simu na kuwaeleza wasafiri usiku ili kesho wawepo bungeni.

“Mwambie asafiri usiku kesho kila mmoja awepo bungeni,” amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad