Spika Ndugai: Waziri Mwambe Ana Majibu ya Hovyo, ni Jeuri




Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wabunge kuhusu majibu aliyoyaita ya kifedhuli yanayotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Geofrey Mwambe na kumtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumfunda.

 

 

Ameyasema hayo leo Alhamisi, Aprili 8, 2021 mara baada ya mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu kumlalamikia Mwambe wakati akichangia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa (2021/22 hadi 2025/26) kwamba alijibiwa vibaya na waziri huyo baada ya kutoa ushauri wakuhusu masoko.

 

 

“Ninayo malalamiko kadhaa ya wabunge kuhusu Waziri Mwambe, wengi wamekuwa wakilalamika kwamba unawapa majibu ya hovyo na kifedhuri pamoja na dharau, Mwambe huyu haelewani na Wabunge wote wa Mkoa wa Mtwara. Nadhani kwa sababu ni mbunge mgeni anadhani kuwa ukiwa waziri ni mtu mkubwa sana bungeni haiendi hivyo.

 

 

“Ana majibu ya ovyo sana hawaheshimu hata wabunge wa kamati yake wanapata tabu jinsi ya kufanya naye kazi. Mhe Waziri Mkuu liangalie hili, analeta ujeuri anadhani Bajeti yake inapitaje hapa, anajiona kuwa Waziri ndio kamaliza kila kitu,” amesema Ndugai.

OPEN IN BROWSER

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad