Mbunge wa Jimbo la Sengerema (CCM), Hamis Hussein Tabasamu, amesema licha ya uwepo wa upungufu wa walimu na waliosomea kuwepo mitaani, Serikali imekuwa haitoi Ajira.
Amesema, “Mimi nafikiri Mtaala wa Ualimu ufutwe katika Vyuo Vikuu kwasababu watu wanapelekwa kusomea Ualimu lakini wanaendelea kuwepo mitaani.
Ameongeza, “Watu wanaenda kusomea Ualimu, una upungufu hautaki kuajiri. Hawa Vijana wetu itakuwaje? Upungufu tunao, lakini hamtaki kuajiri mnakuja na Ajira 6,000. Mimi nashindwa kuelewa hilo jambo.
Aidha, Mhe. Tabasamu amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda Tume kwa ajili ya kwenda kuchunguza mabomba ya majengo ya shule (madarasa, nyumba za walimu na ofisi za walimu) ambazo zinajengwa nchi nzima na kujua hali yake huku akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi wa Serikali wanaosimamia miradi hiyo hawatoi taarifa sahihi kwa kuhofia kupoteza nyadhifa zao.