Taharuki Morogoro: Watu Saba Wakutwa Wakitembea Barabarani Bila nguo


HALI ya taharuki imewakumba wakazi wa kijiji cha Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro baada ya watu saba kukutwa wakitembea barabarani bila nguo huku tukio hilo likidaiwa kuusishwa na imani za kishirikina.

Tukio hilo ambalo picha zake zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii linadaiwa kutokea juzi Aprili 7 mwaka huu ambapo baadhi ya mashuhuda walieleza kuwa watu hao wanadaiwa ni wa familia moja na haijajulikana sababu hasa ya kufanya kitendo hicho


Mmoja wa mashuhuda hao, Idrisa Kamota mkazi wa Mvuha aliieleza Nipashe kuwa siku ya tukio alfajiri wakiwa katika shughuli zao za kawaida walishaangaa kuona kikundi cha watu hao wakiwa katika mstari mmoja bila kuwa na nguo ndipo zikaanza jitihada za kuwazuia wakisaidiana na vyombo vya dola na Serikali.

“Walikuwa watu saba watoto watatu na watu wazima walikuwa wane, tulijaribu kuwazuia wasiendelee na safari bila mafanikio hadi wakaja polisi walipowahoji hawakuongea chochote ikabadi wawavalishe nguo na kuwaelekeza warudi walipo toka” amesema Kamota

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Mvuha Juma Ndunda ambaye pia ni ndugu na familia hiyo, amesema tukio hilo limehusisha familia ya Selemani Mvange akiwa na mke wake, watoto wake wawili na mama yake mkwe pamoja na shemeji zake wawili ambao alikuwa akiishinao nyumba moja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad