Tanzania kushirikiana na Indonesia kukuza Utamaduni

 


Serikali ya Tanzania na Indonesia zimekusudia kukuza ushirikiano katika sekta ya  Utamaduni wa Utalii ili kuongeza ajira kwa vijana wa mataifa yote mawili.


Haya yamebainika Jijini Dodoma baada Mheshimiwa. Innocent Bashungwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kukutana Aprili 23, 2021 na kufanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia Nchini Prof. Ratra Pardede.




Katika mazungumzo hayo serikali ya Tanzania imemwomba Balozi huyo kuunga mkono jitihada za kukuza Sanaa nchini kwa kuchangia katika uwekezaji wa Vifaa vya kuzalishia Filamu na kwakuanzisha Maktaba ambayo itakuwa chini ya Uangalizi wa Chuo na kwa Usimamizi wa Serikali ili kukiendeleza Chuo cha Bagamoyo TASUBA

”Tukiwekeza katika vijana wa sasa tunajenga Taifa imara la kesho na Viongozi bora ambao watakuwa Mabalozi wazuri katika Maendeleo ya Nchi zetu Mbili, Ukizingatia Indonesia ni kati ya Nchi zinanokuwa Kiuchumi na kwa kasi sana Duniani. Jambo hili linaweza likaitoa Tanzania katika Uchumi wa Kati na Kukua zaidi.” Alilisisitiza Waziri Bashungwa.


Mazungumzo hayo yalienda mbali zaidi kwa kusema hatua hii itasaidia Ukuaji wa Sanaa za Filamu Nchini na kuutangaza utamaduni wetu na kuvutia utalii kwa ujumla utakao inua pato la nchi na kuwawezesha vijana ambao ni watashika nyadhifa mbalimbali hapo baadae.


Prof.Pardede alishukuru kwa mazungumzo hayo pia akakili kuvutiwa sana na Utamaduni wa Kitanzania ambao ni kivutio kikubwa sana kwa Taifa la Indonesia.


“Ninatoa mwaliko kwa Waziri Bashungwa Kuhudhulia Tamasha la Utamaduni wa Kindoneshia litakalofanyika Mei 29, 2021 Jijini Dar es Salaam Tanzania ambalo litavijumlisha vikundi mbali mbali vya Kitamaduni vya Nje na ndani ya Nchi ambalo limelenga hasa kuinua Utalii wa Sanaa na Chakula baina ya Tanzania na Indoneshia.” Alisema Balozi huyo


Mazungumzo haya yanakuja baada ya kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya Secta ya Sanaa kutoa ajira zaidi kwa vijana wengi Nchini.


Hadi sasa Nchi ya Indoneshia imetoa nafasi za Ufadhili kwa vikundi vya Sanaa na Utamaduni Nchini kukutana na Wasanii mbalimbali kutoka Nchini Indoneshia ili kubadilishana Ujuzi wa Sanaa na kujiongezea ujuzi binafsi kwa kipindi cha Miezi Sita Nchini Indonesia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad