Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa suala la vifurushi vya bando za internet inafanyia kazi na watoa huduma wameambiwa warekebishe ambapo baadhi yao wameanza.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt.Jabir Bakari amesema TCRA inawafuatilia watoa huduma hao kila siku kuboresha vifurushi kurudi katika mfumo wa zamani.
Amesema kuwa mfumo huo hauwezi kurudi kwa mara moja kinachofanyika kila mtoa huduma anarudisha kwa namna mfumo unavyohitaji.
Dkt.Bakari amewahakikishia watanzania suala la vifurushi litakaa sawa kwani baadhi wameanza kurejesha mfumo wa zamani.
Hata hivyo TCRA imewatoa zuio la mawakala wanaosajili laini za simu na kuwataka kuendelea kwa kuzingatia uweledi.
Mawakala hao wamesema wanaishukuru TCRA kwani walikuwa katika wakati mgumu kwani usajili wanaofanya ndio unafanya kupata fedha kwa ajili ya kuendesha maisha.
Mmoja wa Wakala Yusuf Kiponza amesema wanaishukuru TCRA kuondoa zuio kwani ilikuwa ni sehemu ya ajira kwa kwa vijana.
Nae Athman makwaiya amesema kuwa mfumo usajili kwa sasa umeboreshwa hivyo hakuna mtu anaweza kusajili laini mbili na kusema watazingatia weledi katika kuendelea kuamininiwa na Mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Bakari akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na masuala zuio kuondolewa kwa mawakala wa usajili wa laini za simu pamoja na ufafanuzi wa vifurushi vya Bando.
Kiongozi wa usajili wa Laini simu Athman makwaiya akizungumza namna walivyoipokea suala la kuondolewa kwa zuio lilioanza kutekelezeka Aprili 1.
Wakala Yusuf Kiponza akizungumza kuhusiana namna watavyokuwa watiifu katika kufanya kazi ya usajili baada ya kuondolewa zuio la usajili wa laini za simu.