TCRA yarejesha usajili wa online TV





Siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa na Serikali vifunguliwe, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeondoa zuio la utoaji wa leseni za huduma ya maudhui ya mtandaoni kuanzia jana Ijumaa ya Aprili 9, 2021.
Rais Samia alitoa agizo hilo Aprili 6 alipokuwa akiwaapisha baadhi ya makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wa wizara mbalimbali katika Ikulu ya Dar es Salaam na akaitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa zikiwemo televisheni za mitandaoni.

Taarifa ilitolewa jana na TCRA kwa vyombo vya habari ilisema mamlaka hiyo imeanza kupokea maombi ya leseni na watakaokidhi vigezo wataruhusiwa.

“TCRA inapenda kutoa taarifa kuwa, kuanzia leo Aprili 9 usitishwaji umeondolewa na TCRA imeanza kupokea maombi mapya ya leseni za maudhui ya mitandao,” 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad