Shirikisho la mpira wa miguu nchini ‘TFF’ limefafanua kuwa adhabu aliyopewa makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela kuwa imeegemea kwenye upande wake wa uongozi wa klabu na si kwenye masuala mengine ya kama vile kumzuia asifuatilie taarifa za michezo.
Ndimbo amejibia malalamiko ya makamu mwenyekiti huyo aliyefungiwa kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 5 na faini ya shilingi milioni 7 kuwa, siku tatu zilizopita alisema amezuiwa asisome magazeti ya michezo wala kutazama luninga.
Ndimbo amesema; “Kama ambavyo taarifa ya adhabu ulivyosema, na ni tofauti na alivyoielezea kwamba haruhusiwi hata kusoma magazeti au ikifika kwenye taarifa za michezo azime TV asiangalie. Adhabu aliyopewa ni kwamba majukumu yake ambayo amekuwa nayo ndipo aadhabu ilipoegemea.”
“Asijihusishe na majukumu hayo ya kiuongozi kwa muda huo ila mengine kuhusu kutokusoma magazeti labda alikuwa anafurahisha genge tu.”
(Aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela ambaye kwasa amefungiwa miaka 5).
Ndimbo amesema Mwakalebela amefungiwa kimajukumu ya Uongozi lakini ana nafasi ya kushuhudia michezo viwanjani kama mashabiki wengine.
“Linapokuja suala la kwenda uwanjani hilo sio kujishugulisha na suala la uongozi wa mpira na maana yake umekwenda kama mtazamaji mwingine.”