TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa mikoa minne nchini




Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la kutokea kwa mvua kubwa kuanzia leo Jumamosi Aprili 3, 2021  katika mikoa ya  Dar es salaam, Pwani, Lindi pamoja na kusini mwa Mkoa wa Morogoro.


Taarifa ya matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano iliyotolewa na mamlaka hiyo leo imeeleza kuwa athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.



Imeeleza kuwa Aprili 4, 2021  kutakuwa na uwezekano wa kutokea mvua kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na Lindi.



“Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji. Tafadhali zingatia na ujiandae,” imesema taarifa hiyo.



Pia imesema Aprili 5, 2021 kuna uwezekano wa kutokea mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na Lindi, ambapo athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa baadhi ya shughuli za usafirishaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad