TMA Yatoa Tahadhari ya Mvua Kubwa






MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Aprili 12 hadi Aprili 14, katika Mikoa 15.

 

Taarifa hiyo iliyotolewa na TMA imeonesha mvua hiyo itanyesha Aprili 12 kwenye baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani inayojumuisha Visiwa vya Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara.

 

Pia, mvua inatarajiwa kunyesha Aprili 13, katika Mikoa hiyo na Mikoa mingine ikiwemo Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro.

Aprili 14 itanyesha kwenye baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Katavi, Rukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad