Mwalimu mmoja wa teknolojia ambaye aliwatishia wanafunzi na kuwapeleka katika klabu ya utupu akiwa mlevi chakari wakati wa safari ya shule amepigwa marufuku kufunza kwa miaka mitatu.
Tabia ya Richard Glenn haikuweza kukubalika baada ya kurudishwa nyumbani mapema wakati wa safari ya shule hiyo ya LongRidge kuelekea Costa Rica Julai 2019, Shirika la ualimu liliambiwa.
Bwana Glenn mwenye umeri wa miaka 55 alikiri kufanya makosa na alifutwa kazi mwezi Agosti 2019.
Shule hiyo ya kibinafsi ya Northumberland hugharimu hadi £4,850 kwa muhula mmoja kwa wanafunzi wanaokwenda shule na kurudi nyumbani.
Jopo la adhabu liliambiwa kwamba Bwana Glenn ambaye alikuwa akifunza somo la sayansi ya tarakilishi na amekuwa mkuu wa kidato cha sita tangu 2007, alikua mmoja ya viongozi wa kundi la wanafunzi walio na kati ya umri wa miaka 16 na 18 waliokwenda Costa Rica tarehe tano Julai 2019.
Jopo hilo lilisema kwamba wanafunzi walikuwa wakimtegemea yeye kuongozwa
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,Jopo hilo lilisema kwamba wanafunzi walikuwa wakimtegemea yeye kuongozwa
Jopo hilo lilisema kwamba wanafunzi walikuwa wakimtegemea kwa uongozi nchini Costa Rica.
Alitarajiwa kuwa nchini humo hadi tarehe 28 mwezi Julai , lakini baada ya siku sita alilazimishwa kwenda nyumbani na kiongozi wa safari hiyo kutokana na tabia yake.
Vitendo vyake vilishirikisha:
-Kunywa pombe na wanafunzi
-Kuwaruhusu mwanafunzi mmoja ama zaidi
-kunywa pombe licha ya kuwa chini ya umri wa miaka 18.
-Kutishia kumuua mwanafunzi mmoja
-Kuwaambia wanafunzi hayuko kwenye shida bali wao.
-Baada ya kutaka kumshambulia mwanafunzi mmoja alimbusu katika paji la kichwa chake na kumwambia utakuwa sawa.
Kumpeleka mwanafunzi mmoja ama hata zaidi katika kilabu ya utupu.
Shule hiyo ya kibinafsi karibu na Berwick inatoza £9,800 kwa wanaolala
Shule hiyo ya kibinafsi karibu na Berwick inatoza £9,800 kwa wanaolala
-Kujionesha kwa wanawake katika chumba kimoja cha hoteli,ijapokuwa ilieleweka kwamba hicho hakikuwa kitendo cha unyanyasaji wa kingono.
Jopo hilo lilisema kwamba tabia yake liliwaweka wanafunzi katika hatari.
Liliongezea kwamba hakukuwa na dhamira ya kuwanyanyasa kijinsia wanafunzi hao kwa kuwapeleka katika kilabu hiyo ya burudani , lakini bwana Glenn alikiri haikuwa sawa kwa yeye kushindwa kudhibiti hali hiyo.
Aliongezea kwamba hakuweza kukumbuka kilichotokea kutokana na hali yake ya kulewa chakari .