Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga SC, Juma Mwambusi amesema kuwa wamejiandaa vizuri kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Gwambina FC na wapo tayari kwa kwenda kupambana kuhakikisha wanatoka na pointi tatu.
“Tunajua ni mchezo mgumu na hatuwezi kuwabeza Gwambina FC kutokana na nafasi waliyopo na ukizingatia ushindani wa ligi ni mkubwa msimu huu na wao ni moja kati ya timu bora, wana wachezaji wazuri, wazoefu na wengine wakongwe kwa maa na mchanganyiko na wana Mwalimu vile vile mzuri,” Kaimu Kocha Mkuu Juma Mwambusi
Mwambusi ameongeza ”Wamekuja kutuzuia sisi Yanga, lakini kikubwa tumejiandaa vizuri, kiufundi timu ipo vizuri na tunataraji kwenda kupambana kuhakikisha tunapata pointi tatu katika mchezo wetu wa kesho.”
”Majeruhi ni Mapinduzi Balama, Feisal Salum (Feitoto), Yassin Mustapha wachezaji hao watatu kesho watakakosekana.”
”Tunawaheshimu Gwambina FC, ni timu ambayo inashiriki Ligi Kuu ikija ikihitaji kutuzuia, Timu yangu haitoweza kwenda kukaa nyuma tutashambulia, hii yote ni kuhakikisha tunatafuta nafasi nyingi za kufunga na kutumia hizo nafasi tunazozitengeneza.”