Tundu Lissu "Katika Inaruhusu Mikutano ya Kisiasa Ila Polisi Nao Wana Sheria ya Kukataza



Tundu Lissu amesema Katiba inaruhusu mikutano na maandamano ya Kisiasa lakini Polisi wana #Sheria mpya ya kukataza Mikutano. Katika mfumo wa Vyama vingi bado Sheria za tawala za Mikoa ni za Chama Kimoja


Ameongeza kuwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaweka Watu ndani, Rais ana Mamlaka ya kuweka watu kizuizini bila kupelekwa Mahakamani na Sheria Kandamizi hazikufanyiwa marekebisho Mfumo wa Vyama vingi ulipokuja


Asema "Mfumo wa Uchaguzi ni Mfumo wa Chama kimoja ya 1985. Ulitungwa kwa mazingira ya Chama kimoja tangu 1962 hadi leo. Tuliingia Vyama vingi bila #Demokrasia. Vyama Vyote vilitakiwa kusajiliwa kama CCM ilivyosajiliwa"


Pia, "Kwa miaka mitano Rais anasema kamata huyu unakamatwa. Nilikamatwa mara 8 kwa mwaka, Nikiuliza kwanini nakamatwa? Naambiwa ni amri kutoka juu. Sijawahi ambiwa nani katoa hiyo amri kutoka juu. Ukweli wa amri kutoka juu ni amri za Ikulu".

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad